Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.
Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa. Yanayochochea zinaa ni pamoja na mavazi yasiyozingatia sheria ya Kiislamu; michanganyiko ya wanaume na wanawake isiyozingatia sheria ya Kiislamu; michezo, miziki, ngoma, nyimbo na mengineyo yanayochochea zinaa.
"… Hakika hiyo zinaa ni uchafu (mkubwa) na ni njia mbaya (kabisa)" (17:32)
Uchafu na ubaya wa zinaa unadhihirika wazi kwa wahusika binafsi na kwa jamii kwa ujumla katika maeneo yafuatayo:
(i)Magonjwa ya zinaa ukiwemo UKIMWI, ambayo hudhoofisha afya na kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
(ii)Kuporomosha maadili ya jamii. Watu wazinifu hawana haya, ni watovu wa nidhamu, walaghai, waongo, wabinafsi na wapupia machafu ya kila namna.
(iii)Zinaa huondosha umuhimu na heshima ya ndoa.
(iv)Kuvunja ndoa na kusababisha matatizo ya kifamilia.
(v)Husababisha watoto wa mitaani na kuingiza jamii katika janga la wahuni, wala unga, matapeli, majambazi pamoja na kusababisha kundi kubwa la vijana wasio na uwezo wa kufanya lolote.
Umeionaje Makala hii.. ?
Ukizingatia maana halisi ya dini, kuwa dini ni utaratibu wa maisha, utadhihirikiwa kuwa umbile la mwanaadamu ni la kidini.
Soma Zaidi...Nguzo za Imani (EDK form 2:. Dhana ya elimu ya uislamu
Soma Zaidi...Mwanaadamu ametunukiwa neema mbali mbali na Mola wake kuliko viumbe wengine wote kama tuanvyojifunza katika aya mbali mbali za Qur'an.
Soma Zaidi...“Basi vyote hivi mlivyopewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilicho kwa Mwenyezi Mungu ni bora na cha kudumu (milele).
Soma Zaidi...Wakatibmeingibe Allah anapotaka kuwasiliana na wanadamu hutuma Malaika wake.
Soma Zaidi...