Kujiepusha na kuua nafsi bila ya Haki
Kuua nafsi bila ya Haki, ni kuiua nafsi isiyo na kosa linalostahiki hukumu ya kifo.
(d) Kujiepusha na kuua nafsi bila ya Haki.
Kuua nafsi bila ya Haki, ni kuiua nafsi isiyo na kosa linalostahiki hukumu ya kifo. Hata kama mtu amefanya kosa la kustahiki kuuliwa, hatauliwa kwa mtu binafsi kuchukua sharia mkononi bali itabidi afikishwe mbele ya Kadhi na ahukumiwe kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu.
Si nafsi ya binaadamu tu iliyoharamishwa kuuliwa pasina haki bali hata nafsi za viumbe vingine vyote ikiwa ni pamoja na wanyama wakubwa na wadogo na mimea. Kwa mfano tunaruhusiwa kuwaua wanyama kwa ajili ya manufaa kutoka kwao au kwa ajili ya kujikinga na madhara yao dhidi ya binaadamu. Pia haturuhuswi kukata au kuteketeza mimea ovyo ovyo pasina haja maalumu na kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira.
β Wala msiwaue watoto umasikiniβ¦β(1 7:31)
Kiutendaji kuwaua watoto kwa kuogopa umasikini si lazima kuishia kwenye kuwaua watoto waliokwisha zaliwa bali hata kuzuia mimba isitokee, kutoa mimba au kufunga kizazi bila ya sababu ya msingi ya kiafya ni katika kuua watoto. Na katika aya hizi Allah (s.w) anatahadharisha:
"β¦ Kwa yakini kuwaua ni khatia kubwa". (17:31)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) π2 Kitabu cha Afya π3 web hosting π4 Kitau cha Fiqh π5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina π6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu
Ni upi mgawanyo sahihi wa elimu katika uislamu? Nini naana ya elimu ya muongizo. Je elimu ya mazingiravmaana yakeni nini. Ni upi utofauti wa elimu ya muongozo na elimu ya mazingira?
Soma Zaidi...Maamrisho ya kushikamana nayo
Yale tunayoamrishwa kushikamana nayo ni haya yafuatayo: (i)Kumuabudu Allah (s.
Soma Zaidi...Kwa namna gani Allah huwasiliana na wanadamu kwa kupitia ndoto.
Ndoto za kweli ni moja kati ya njia ambazo Allah huwasiliana na wanadamu.
Soma Zaidi...