Kujiepusha na kukaribia zinaa

Kujiepusha na kukaribia zinaa

Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.

Kujiepusha na kukaribia zinaa

(e)Kujiepusha na kukaribia zinaa



Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa. Yanayochochea zinaa ni pamoja na mavazi yasiyozingatia sheria ya Kiislamu; michanganyiko ya wanaume na wanawake isiyozingatia sheria ya Kiislamu; michezo, miziki, ngoma, nyimbo na mengineyo yanayochochea zinaa.



"… Hakika hiyo zinaa ni uchafu (mkubwa) na ni njia mbaya (kabisa)" (17:32)



Uchafu na ubaya wa zinaa unadhihirika wazi kwa wahusika binafsi na kwa jamii kwa ujumla katika maeneo yafuatayo:



(i)Magonjwa ya zinaa ukiwemo UKIMWI, ambayo hudhoofisha afya na kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
(ii)Kuporomosha maadili ya jamii. Watu wazinifu hawana haya, ni watovu wa nidhamu, walaghai, waongo, wabinafsi na wapupia machafu ya kila namna.
(iii)Zinaa huondosha umuhimu na heshima ya ndoa.
(iv)Kuvunja ndoa na kusababisha matatizo ya kifamilia.
(v)Husababisha watoto wa mitaani na kuingiza jamii katika janga la wahuni, wala unga, matapeli, majambazi pamoja na kusababisha kundi kubwa la vijana wasio na uwezo wa kufanya lolote.




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF
Views: 3148

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 web hosting     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉6 Dua za Mitume na Manabii    

Post zinazofanana:

Mitume wa uongo

Wafuatao ni baadhi ya wale waliodai utume wakati Mtume (s.

Soma Zaidi...
Mtazamo wa Uislamu juu ya maana ya dini

Uislamu unaitazama dini katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu. Hii ni tofauti na mtazamo wa kikafiri juu ya dini.

Soma Zaidi...
Kumuamini malaika wa mwenyezi Mungu...

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...