Sababu za maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa

Sababu za maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa

Utajifunza sababua zinazopelekea kuhisi maumivu makali ya tumbo baada ya kumaliza tendo la ndoa

Download Post hii hapa

Sababu za maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa

MAUMIVU YA TUMBO BAADA YA TENDO LA NDOA




Mara nyingi maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa sio tatizo sana kiasi cha kuogopa. Kwani hali hii husababishwa na gesi iliyoppntumboni mama kama uume ulikuwa ukiingia ndani sana, na hii hutokea endapo uume ni mrefu sana ama mtindo uliotumika katika tendo la ndoa. Tatizo la kupatwa na maumivu wakati wa tendo la ndoa ama baada hutambulika kama dyspareunia.



Inakadiriwa kuwa asilimia 10 mapka 20 ya wanawake huweza kusumbuliwa na tatizo hili. Ila pia tatizo hili si kwa wanawake tu hutokea pia kwa wanaume, ila kwa kiasi kidogo yapata lamda asilimia 5. lakini tatizo hili linatibika bila ya wasi hivyo si vyema kuendelea kuteseka.



Sababu za maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa.
Tofauti na sababu ya ya gesi ama uume kuingia ndani sana, tatizo hili linaweza kusababishwa na mambo yafuatayo:-



1.Fikra, hisia na mawazo ya mtu. Hii hutokea kama mtu ana misongo ya mawazo kibao, ama ana woga juu ya tendo la ndoa ama mahusianao yake na ya mwenzie sio mazuri lamada amembaka ama kumlazimisha, haya yote yanaweza kutengeneza mazingira ya kuumwa na tumbo baada ya tendo.



2.Endapo tendo la ndoa litafanyika kwa kiasi kuwa uume uliingia ndani sana. Hii inaweza kusababisha maumivu ya tumbo, ila ni ya muda mfupi na yataweza kuondoka baada ya kupumzika. Ni vyema kubadili mikao ama kupunguza kukandamiza sana uume.



3.Wakati mwingine hali huweza kutokea endapo mwanamke ameingia kileleni. Wakati wa kufika kileleni misuli inayozungukia mfumo wa uzazi, maeneo ya kiunoni na nyonga misuli hii kusinjaa na kujikaza na kusababisha maumivu ya chini ya tumbo. Hali jii kitaalamu hufahamika kama dysorgasmia.



Watu wanaosumbuliwa sana tatizo hili ni:-
A.Wajawazito
B.Wenye matatizo kwenye ovari
C.wenye mashambulizi ya kwenye mfumo wa uzazi (PID)
D.Wenye matatizo kwenye korodani.



4.Gesi; wakati wa kupushi uume ndani unaweza kupushi hewa kuingia ndani ya tumbo. Sasa kama hewa hii itanaswa sehmemu humo ndani inaweza kusababisha maumivu ya tumbo kwa juu ama kifuani. Mtu anaweza kuhisia kama gesi inatembea tumboni na maumivu haya yanaweza kuelekea maeneo mengine ya mwili.



5.Kama mtu anasumbuliwa na UTI
UTI inaweza kuwa ni katika sababu za maumivu haya. Mtu pia anaweza kuhisi dalili kama
A.Maumivu wakati wa kukojoa kama anaungua
B.Kukojoa mara kwa mara
C.Mkojo kuwa mchafu
D.Kuwa na damu kwenye mkojo
E.Maumivu ya mkundu.



6.Kuwa na maradhi ya ngono kama gonoria na chlamydia. Pia mtu anaweza kuona dalili kama:
A.Kutoa harufu mbaya sehemu za siri
B.Kutokwa na uchafu sehemu za siri
C.Maumivu wakati wa kukojoa



7.Kama mfuko wa uzazi umeinama, hii inaweza kupelekea kuguswa kwa mfukowa uzazi wakati wa tendo la ndoa hivyo kupelekea maumivu



8.Kama kunashida kwenye ovari




9.Kama kuna uvimbe kwenye kizazi. Dalili zake ni kama
A.Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi
B.Hedhi kutokata ndani ya siki 7
C.Kukosa choo
D.Maumivu ya miguu ama mgongo



10.Kama mirija ya falopia imeziba.



11.Kama mwanaume ana maradhi kwenye mfumo wa uzazi.





                   



Download Post hii hapa

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Uzazi Main: Afya File: Download PDF Views 9293

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

NAMNA YA KUBORESHA MBEGU ZA KIUME, NA VYAKULA VYA KUBORESHA NGUVU ZA KIUME
NAMNA YA KUBORESHA MBEGU ZA KIUME, NA VYAKULA VYA KUBORESHA NGUVU ZA KIUME

Njoo ujifunze vyakula vya kuboresha mbegu za kiume na nguvu za kiume.

Soma Zaidi...
Je inaweza ukaingia period wakati unaujauzito?
Je inaweza ukaingia period wakati unaujauzito?

Ukiwa mjamzito unaweza kushuhudia kutokwa na damu. Je damu hii ni ya hedhi?

Soma Zaidi...
Hiv n kweli majivu hutoa mimb ya siku moja hadi wiki moja
Hiv n kweli majivu hutoa mimb ya siku moja hadi wiki moja

Inashangaza sana, wakati wengine wanahangaika kutafutavijauzito kwa gharama yoyote ile, kuna wengine wanataka kutoa ujauzito kwa gharama yeyote ile. Unadhani njia za kienyeji sa kutoa mimba ni salama?

Soma Zaidi...
Post hii inahusu zaidi umuhimu wa kondo la nyuma
Post hii inahusu zaidi umuhimu wa kondo la nyuma

Kondo la nyuma ni sehemu ya mwili wa mama anapokuwa mjamziti,kondo la nyuma husaidia katika kazi mbalimbali katika ukuaji wa mtoto.

Soma Zaidi...
Maandalizi ya mama mjamzito kwa ajili ya kujifungulia.
Maandalizi ya mama mjamzito kwa ajili ya kujifungulia.

Postii inafundisha maandalizi ya mama kwa ajili ya kujifungulia hii Ni muhimu Sana kwa wale ambao hawajawahi kujingua Ni mara yao ya kwanza wanatakiwa kujua na kuelewa vifaa na mahitaji kujifungulia na kwa wale wanaohudhuria clinic huwa wanafundisha.

Soma Zaidi...
Kuwepo kwa maziwa wakati wa ujauzito.
Kuwepo kwa maziwa wakati wa ujauzito.

Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa maziwa kwa akina Mama wakati wa ujauzito ni kawaida kwa sababu ya kuzaliwa kwa homoni ambayo usaidia kutoa maziwa.

Soma Zaidi...
TATIZO LA KUVIMBA KWA USO NA MIGUU KWA WAJAWAZITO
TATIZO LA KUVIMBA KWA USO NA MIGUU KWA WAJAWAZITO

KUVIMBA VYA MIGUU KWA WAJAWAZITO Kuvimba kwa miguu ni hali inayowapara wengi katika wajawazito.

Soma Zaidi...
Changamoto kubwa za tendo la ndoa kwa wanaume
Changamoto kubwa za tendo la ndoa kwa wanaume

Posti hii inahusu zaidi changamoto ya tendo la ndoa kwa wanaume,wanaume wamekuwa wakipata changamoto ya tendo la ndoa na kuwafanya kushindwa kujiamini na kukosa kabisa raha kwenye maisha yao

Soma Zaidi...
Kushiriki tendo la ndoa wakati wa ujauzito
Kushiriki tendo la ndoa wakati wa ujauzito

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kushiriki tendo la ndoa wakati wa ujauzito faida na hasara zake

Soma Zaidi...