Sababu za mimba ya miezi 4-6 kutoka.

Posti hii inahusu zaidi sababu za mimba ya miezi kuanzia minne mpaka sita kutoka , Kuna kipindi mimba kuanzia miezi mimne mpaka sita utoka kwa sababu mbalimbali.

Sababu ya mimba kuanzia miezi 4_6 kutoka.

1. Kuwepo kwa lishe mbaya.

Kuna wakati mwingine akina Mama wakibeba mimba uanza kula mambo ya ajabu ambayo ni pamoja na kula udongo, mkaa,pemba na vitu kama hivyo na kuanza kuacha kutumia vyakula vya maana ambavyo vinaleta afya kwenye miili yao , kama vile folic acid na vyakula vyenye madini.

 

2. Kuwepo kwa matatizo kwenye tezi.

Kuna wakati mwingine kitendo cha kuwepo kwa tezi bila kitibiwa usababisha mimba kutoka hasa kwenye kipindi cha miezi minne mpaka sita.

 

3. Pia kama Kuna maambukizi kwenye njia ya uzazi.

Kwa sababu magonjwa mengine mama uyapata akiwa tayari ana mimba na pia kwa kuwa akina Mama wengi upima siku za mwanzo kwa hiyo usababisha mimba kutoka.

 

4. Pengine msongo wa mawazo.

Kuna kipindi kunakuwepo na msongo wa mawazo kwa akina Mama wakiwa na mimba na kusababisha mpaka mimba kutoka, msongo wa mawazo inawezekana ni kwa sababu Mama hapati matumizi ya kutosha au mme wake anamsumbua na mambo kama hayo.

 

5. Uzito mkubwa kupita kiasi.

Nii vizuri kupunguza Uzito wakati wa ujauzito Ili kuepuka tatizo la mimba kuharibika.

 

6. Kuwepo kwa maambukizi kwenye mlango wa kizazi.

Na hili ni tatizo kwa Sababu usababisha kuenea kwenye sehemu mbalimbali kwa mtoto na sehemu aliyojishikiza na kusababisha mimba kutoka.

 

7. Kulegea kwa mfuko wa mimba.

Kuna kipindi kwa sababu mbalimbali utokea ambapo usababisha mfuko wa uzazi kulegea na kusababisha mimba kutoka.

 

8. Shinikizo la damu kuwa juu.

Kwa hiyo akina Mama kila udhulio wanapaswa kupima kiwango cha shinikizo la damu Ili kuepuka mimba kutoka.

 

9. Matumizi ya dawa pasipo daktari.

Na hilo ni tatizo ambapo madawa mengine unakuta hayaruhusiwi kutumiwa na akina Mama wakati wa ujauzito ila wao wanatumia tu.

 

10. Matumizi ya chakula chenye Sumu.

Kuna wakati mwingine akina Mama wanaweza kutumia vyakula vyenye Sumu na kusababisha mimba kutoka.

 



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/21/Thursday - 07:24:59 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 8132


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-