Hizi ni siku hatari kwa mwanamke ambazo ni ahisi kwake kubeba mimba, siku nitakueleza ni zipi na ni zipi sifa zake
SIKU ZA KATARI NA SIKU ZA KUSHIKA MIMBA.
Kila mwanamke ana siku yake ambayo ni hatari zaidi kushika mimba. Siku hii inaweza kufanana na mwanamke mwingine ambaye anafanana naye mahesabu. Hata hivyo wanaweza kutofautiana kutokana na vyakula, maumbile na hali za maisha. Hapa nitakuletea orodha ya siku hatari za mwanamke.
Nini maana ya siku hatari?
Hizi ni siku ambazo mwanamke anakadiriwa kupata ujauzito. Ni mfululizo wa siku ambazo makadirio ya mwanamke kupata ujauzito ni mkubwa kuliko siku nyingine. Kabla ya kuzijuwa siku hizi kwanza hakikisha unajuwa vyema idadi ya siku mwanamke anazokwenda hedhi. Wanawake wanakwenda hedhi ndani ya mzunguruko unaoanzania siku 21 mpaka 35. hii inamaana kuna am,bao siku zao ni nyingi na wengine ni kidogo.
Sasa ni ipi siku hatari kwa mwanamke, siku ambayo mawanamke atapata ujauzito?. siku hii nitakuorodheshea, ila kwanza nataka tu nikujuze kwa ufupi sifa ya siku hiyo. Kwa nini, ni kwa sababu siku hizi zipo nyingi na zote ni hatari kwani zinaweza kuleta mimba. Ila katika hizo ipo ambayo ni hatari zaidi. Siku hiyo ina sifa hizi:-
1.Mwili wa mwanamke katika siku hii utakuwa na joto kulinganisha na siku zilizopita. Kwa urahisi unaweza kugunduwa kama unatumia kipima joto. Ila ukiwa makini unaweza kujigunduwa kama joto lako limepanda. Hakikisha ongezeko hiki ka joto hakiambatani na shida nyingine za kiafya kama maradhi.
2.Uteute unaopatikana kwenye shingo ya kizazi utakuwa umeongezeka na ni wenye kuteleza kama vile majimajiya yai lililopasuliwa. Kama utaingizakidole ndani zaidi ya uke unaweza kuupata kwenye kidole chako.
3.Siku hii hamu ya kushiriki tendo la ndoa nikubwa kuliko siku yingine. Hii haina haja ya kuielezea. Kama mwanamke homoni zake hazina shida basi lakima kutakuwa na siku ambayo atahitaji sana kushiriki ngono kuliko siku nyingine.
Nitaijuwaje siku hatari, ya kupata mimba?
Kikawaida yai hutolewa (ovulation) kwa makadiria ya siku 12 mpaka 16 kabla ya kupata hedhi nyingine. Yaani unaweza kuhesabu kabla ya kuingia hedhi siku 12 nyuma, kisha toa siku 4 mnyuma ndani ya siku nne zizi ndizo yai hutolewa. siku hizi ndizo moja wapo yai hutolewa. Kwa mfano:--
1.Mwanamke mwenye mzunguko wa siku 21, sasa tunatoa siku 12 nyuma kabla ya kuingia hedhi (21 - 12 = 9) kisha toa nne nyuma (9-4=5) basi mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 5 na 9 katika siku zake.
2.Mwanamke mwenye mzunguruko wa siku 32: tunaanza kutoa siku 12 nyuma kabla ya kupata hedhi yake (32-12=20) tonatoa siku nne tena nyuma (20-4=16) kwa hiyo mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 16 mpaka 20
Tumia mfano huu kwa kuitafuta siku yako ya kupata ujauzito. Kama utakuwa na maoni na maswali wasiliana nasi hapo chini.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
Somo hili linakwenda kukuletea tiba mbadala ya fangasi wa uumeni
Soma Zaidi...Kama na wewe una tatizo la kupitiliza siku zako za hedhi hli ya kuwa huna ujauzito, soma post hii ina majibu yako.
Soma Zaidi...Tezidume ni moja ya magonjwa hayari yanayotokea katika mwili wa mwanaume.Hapa nimekuandalia sababu za kutokea kwa tezi dume.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi upungufu wa homoni ya estrogen na dalili zake, aina hii ya homoni ikipungua mwilini uleta madhara na matatizo mbalimbali kwenye mwili.
Soma Zaidi...Habari DoktaNikuulize kituu?
Soma Zaidi...Kipimo cha mimba kwa mkojo kimekuwa kikitumika sana kuangalia ujauzito. Kipimo hiki kinapotumika vibaya kinaweza kukupa majibu ya uongo. Kuwa makini na ujue muda sahihi.
Soma Zaidi...Kamaumeshawahi kujiuliza kuhusu kutokwaba damu tofautivna siku za hedhi, base mwaka hii ni kwaajiki yako.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi madhara ya kutumia madawa ya shida ya upumuaji, ni madhara madogo madogo ambayo utokea kwa watumiaji wa matatizo ya kupumua.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo ujitokeza kama kuna Maambukizi yoyote kwenye kitovu cha mtoto mdogo, kwa kawaida kitovu cha mtoto kama kiko vizuri kinapona kwa mda mchache na kinakauka mapema iwezekanavyo bila kuwa na tatizo lolote ila kama kuna Dal
Soma Zaidi...Vyakula hivi hapasi kuvila mwanamke mwenye ujauzito kwa kiasi kikubwa, hasa yule mwenye mimba chaga
Soma Zaidi...