image

Siku za kupata mimba

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kupata mimba

Siku za kupata mimba.

Kupata mimba ni majaaliwa kama waswahili walivyozoea kusema. Lakini unaweza kufanya jitihada binafsi ili kuonyesha uhitaji wako. Je na wewe ni muhanga wa tatizo hili la kutopata ujauzito? Makala hii ni kwa ajili yako, hapatutaona njia za kuweza kuzijuwa siku za kupata mimba. Pia tutaona dalili za siku hizo.

 

 

Mimba huweza kuingia siku ambayo yai litakutana na mbegu ya kiume kwenye mirija ya falopia kwenye tumbo la uzazi la mama. Yai la mwanamke kuzalishwa kwenye ovari. Mwanamke ana ovari mbili, moja upande wa kulia na nyingine kushoto. Hizi mbili hupeana zamu ya kutoa mayai. Yaani kama mwezi huu limetoa hili na nyingine itatoa mwezi ujao.

 

Tafiti zinaonyesha kuwa yai huweza kuanza kukomaa kuanzia siku ya 10 toka kupata hedhi mpaka siku ya 14. hii ni kwa wanawake wengi. Ila si wote. Kikawaida yai hutolewa (ovulation) kwa makadiria ya siku 12 mpaka 16 kabla ya kupata hedhi nyingine. Yaani unaweza kuhesabu kabla ya kuingia hedhi siku 12 nyuma, kisha toa siku 4 mnyuma ndani ya siku nne zizi ndizo yai hutolewa. siku hizi ndizo moja wapo yai hutolewa.

 

Kwa mfano:--

1.Mwanamke mwenye mzunguko wa siku 21, sasa tunatoa siku 12 nyuma kabla ya kuingia hedhi (21 - 12 = 9) kisha toa nne nyuma (9-4=5) basi mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 5 na 9 katika siku zake.

 

2.Mwanamke mwenye mzunguruko wa siku 32: tunaanza kutoa siku 12 nyuma kabla ya kupata hedhi yake (32-12=20) tonatoa siku nne tena nyuma (20-4=16) kwa hiyo mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 16 mpaka 20.

 

3.Mwanamke mwenye siku 28: 28-12 = 16 kisha toa siku 4 nyuma 16 - 4 = 12. hivyo siiku ambazo yai hukomaa kwa mwenye siku 28 ni kati ya 12 mpaka 16.

 

Sasa baada ya kuzijua siku hizi ambazo yai hukomaa, inabidi ufahamu kuwa yai la mwanamke huweza kuishi kati ya masaa 12 mpaka 24 toka kukomaa (ovulation). kwa upande mwingine mbegu za kiume huisho kati ya siku 3 mpaka 5. hivyo ujauzito unaweza kutungwa kwa mbegu ambayo ilikuwepo toka siku tatu zilizopita.

 

 

Mimba hutokea pindi mbegu ya kiume (sperm) inapokutana na yai la mwanamke (ova) na kuungana kwa pamoja kutengeneza selli moja iitwayo zygote. Seli hii hukuwa na kujakuwa mtoto kamili. Kawaida kitendo hiki hufanyika ndani ya masaa 12 toka yai kukomaa na kuletwa kwenye mirija ya falopian. Baada ya mimba kutungwa itabakia pale kwa masaa kama matatu, kisha huanza kusafirishwa na kupelekwa kwenye tumbo la mimba ambapo huku litabakia mpaka mtoto kuzaliwa.

 

Mwanamke hutoa yai moja kila mwezi kutoka katika ovari moja. Kuna wakati mwanamke huenda akatowa mayai zaidi ya moja, hali hii si kawaida. Yai hili linaweza kuwa hai ndani ya masaa 12 mpaka 24. hutokea pia likaweza kuwa hai mpaka masaa 48. ndani ya muda huu yai ni lazima likutane na mbegu ya kiume ili mimba itungwe. Kipindi hiki kitaalamu kinajulikana kama fertile window.

 

Mbegu ya mwanaume huweza kudumu kuwa hai ndani ya siku 5, ndani ya siku hizi mbegu hizi huwa zipo hai hivyo zinaweza kurutubisha yai. Mwanaume huto zaidi ya mbegu milioni 300 ejaculation moja. Katika mbegi hizi mbegu moja ndio hutakiwa kuungana na yai.

 

Siku za mwanamke kuweza kuwa kati ya 21 mpaka 35 inategeme na mwanamke. Kikawaida walio wengi siku zao ni 28. katika siku hizi zipo siku 6 tu ambazo mwanamke anaweza kupata ujauzito. Siku hizi huanzia siku ya 11,12,13,14,15 na 16. katika siku hizi siku ya 14 ndio ambayo huaminika zaidi kuwa yai hutolewa ziku hii. Ni vyema kukutana kimwili katika siku hizi kwa wanaotafuta ujauzito. Sio lazima pia kufululiza inawezekana kuruka ila nivyema kutoikosa siku ya 13 na 14.






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2472


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Nahitaji kufaham siku ya kumpatia mimba make wangu, yeye hedhi yake ilianza talehe22
Je na wewe ni moja kati ya wake ambao wanahitajivkujuwa siku za kupata mimba. Ama siku za competes mwanamke mimba. Post hii ni kwa ajili yako. Soma Zaidi...

Jinsi ya kuacha kupiga punyeto.
Post hii inakwenda kukupa njia za kukusaidia kuacha punyeto. Soma Zaidi...

Faida na hasara za Kufunga kizazi kwa wanawake.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Kufunga kizazi kwa wanawake. Soma Zaidi...

Tatizo la kutokwa na utelezi wenye damu baada ya hedhi
Posti hii inahusu zaidi dalili mbalimbali za kutokwa na damu baada ya hedhi hili ni tatizo ambalo uwapata wanawake wengi pamoja na akina Mama kwa sababu ya kutokwa na damu yenye utelezi baada ya hedhi. Soma Zaidi...

Siku za hatari, siku za kubeba mimba
Hizi ni siku hatari kwa mwanamke ambazo ni ahisi kwake kubeba mimba, siku nitakueleza ni zipi na ni zipi sifa zake Soma Zaidi...

Siku za kupata mimba
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kupata mimba Soma Zaidi...

Huduma kwa wanaotoa damu yenye mabonge
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia wanaotoa hedhi yenye mabonge, ni tatizo ambalo uwakumba wasichana hata wanawake wakati wa hedhi. Soma Zaidi...

Sababu za Kukoma hedhi (perimenopause)
Kukoma hedhi hufafanuliwa kuwa hutokea miezi 12 baada ya kipindi chako cha mwisho cha hedhi na huashiria mwisho wa mizunguko ya hedhi. Kukoma hedhi kunaweza kutokea katika miaka ya 40 au 50. Kukoma hedhi ni mchakato wa asili wa kibaolojia. Ingawa pia in Soma Zaidi...

Hatua za ukuwaji was mimba na dalili zake
Somo hili linakwenda kukuletea hatua za ukuaji mimba na dalili zake Soma Zaidi...

SABABU ZA KUTOKA KWA MIMBA (sababu za kuharibika kwa ujauzito)
Tafiti zinaonesha kuwa karibia asilimia 10% mpaka 25% ya wanawake wanaopata ujauzito, mimba zao hutoka. Soma Zaidi...

Sababu za kupasuka kwa mfuko wa kizazi
Posti hii inahusu zaidi sababu za kupasuka kwa mfuko wa uzazi hasa mama anapokalibia kujifungua. Soma Zaidi...

Kupima ujauzito kwa kutumia chumvi, sukari na sabuni
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupima mimba kwa kutumia chumvi sukari na sabuni Soma Zaidi...