NAMNA YA KUSWALI SEHEMU YA KWANZA

Mtume (s.

NAMNA YA KUSWALI SEHEMU YA KWANZA

Mtume (s.a.w) ametuagiza katika Hadith maarufu kuwa tuswali kama alivyokuwa akiswali. Hivyo katika sehemu hii tutajitahidi kuonesha utekelezaji wa swala hatua kwa hatua kwa kurejea Hadith Sahihi za Mtume (s.a.w):

1. Nia na Takbira ya kuhirimia
Nia ni kudhamiria moyoni kuwa unaswali, swala unayoikusudia kisha unaanza swala kwa kusema: “Allaahu Akbar” Allah ni Mkubwa kwa kila hali”. Wakati wa kuhirimia swala ni sunnah kuinua viganja vya mikono,mkabala na mabega. Kuhusu unyanyuaji wa mikono mkabala na mabega imeripotiwa kuwa Mtume (s.a.w) alikuwa akifanya hivyo katika sehemu nne tofauti:
1. Wakati wa kuhirimia swala (kuanza swala).
2. Wakati anaposema Allaahu Akbar kwa ajili ya rukui.
3. Wakati anaposimama kutoka kwenye rukuu.
4. Wakati anaposimama kutoka kwenye tahiyyatu ya kwanza ili kuendelea na rakaa ya tatu.

Hii tunaipata katika Hadith aliyosimulia Abdullah bin ‘Umar kuwa: “Mtume (s.a.w) aliposimama kwa ajili ya swala alinyanyua mikono yake mkabala na mabega yake na kisha kuhirimia (kusema Allahu Akbar). Alipotaka kurukuu alinyanyua mikono kama alivyofanya kwanza na aliposimama kwa ajili ya itidali alifanya hivyo hivyo na alisema Allah anamsikia yule anayemsifu. (Bukhari, Muslim na Bayhaqi). Nafa’a(r.a) ameeleza kwamba Ibn ‘Umar (Abdullah)(r.a) aliposimama kwa ajili ya rakaa ya tatu alikuwa akinyanyua mikono; jambo ambalo alilihusisha na Mtume (s.a.w). (Bukhari, Abu Dawud, Nasai).

Baada ya kuhirimia swala mwenye kuswali hushusha mikono yake na kuiweka kifuani, mkono wa kulia ukiwa juu ya mkono wa kushoto kwa mujibu wa Hadith zifuatazo: Hulab At-Tai(r.a) amesimulia: “Nilimuona Mtume (s.a.w) akiswali hali ameweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto juu ya kifua chake.” (Ahmad na At-Tirmidh)

Naye Wail bin Hijr (r.a) ameripoti: “Niliswali pamoja na Mtume (s.a.w) na aliweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto juu ya kifua chake”. (Ahmad na At-Tirmidh).

Imamu Abu Dawud na Nasai wamepokea kutoka kwa Ibn Khuzaimah kuwa Mtume (s.a.w) alipokuwa akiswali alikuwa akiweka mkono wake wa kulia juu ya kiwiko (wrist) cha mkono wa kushoto na sehemu ya mkono inayofuatia kiganja .


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Jiunge nasi WhatsApp
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1876

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉5 web hosting    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Taratibi za malezi ya watoto wadogo baada ya talaka katika uislamu

Endapo mke na mume wameachana na hali ya kuwa mke ana watoto wachanga. Je uislamu unasemaje kuhusu taratibu za malezi?

Soma Zaidi...
Kujitwaharisha kutokana na najisi

Post hii itakufundisha namna ya kutwaharisha Najisi.

Soma Zaidi...
Jinsi ya kujitwaharisha Najisi hafifu na najisi ndogo

Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kujitwaharisha kutokana na najisi hafifu na najisi ndogo.

Soma Zaidi...
Dhana ya haki na uadilifu katika uislamu

Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Umuhimu na msisitizowa zakat na sadaqat katika uislamu

Nguzo za uislamu,umuhimu na msisitizowa zakat na sadaqat katika uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...