picha

Kusimamisha Swala

Kusimamisha Swala.

Kusimamisha Swala

Kusimamisha Swala.
Maana ya Kusimamisha Swala Kusimamisha swala ni tofauti na kuswali. Kuswali ni kufanya vitendo vya swala kama vile kusimama, kurukuu, kuitidali, kusujudu, n.k.
Kusimamisha swala ni kuitekeleza swala kwa kuchunga na kutekeleza kwa ukamilifu yafuatayo:
(i) Sharti zote za swala.
(ii) Nguzo zote za swala.
(iii) Kuwa na khushui (unyenyekevu) wakati wote wa kutekeleza sharti na nguzo za swala.

Mtu akiswali bila ya kuzingatia na kutekeleza kwa ukamilifu mambo haya matatu, ataonekana kuwa kaswali, lakini atakuwa hajasimamisha swala na atastahiki kuadhibiwa vikali na Mola wake kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo: Basi adhabu kali itawathibitikia wanaoswali, ambao wanapuuza swala zao (kwa kutozisimamisha), ambao hufanya ria (107:4-6).

Kupuuza swala ni pamoja na kutotekeleza ipasavyo sharti za swala, nguzo za swala, na kutokuwa na unyenyekevu wakati wa kutekeleza sharti na nguzo za swala. Hivyo, swala inayokubalika mbele ya Allah (s.w) ni ile iliyosimamishwa kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo: Hakika wamefuzu waumini ambao katika swala zao ni wanyenyekevu. (23:1-2) Na ambao swala zao wanazihifadhi. (23:9) Kuhifadhi swala ni kutekeleza kwa ukamilifu sharti na nguzo zote za swala.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Jiunge nasi WhatsApp
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 2210

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 ai web app    👉2 web hosting    👉3 Dua za Mitume na Manabii    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana:

Wenye ruhusa za kutofunga ramadhan

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Swala ya witiri na faida zake, na jinsi ya kuiswali

Hapa utajifunza jinsi ya kuswali swala ya witiri na faida zake kwa mwenye kuiswali.

Soma Zaidi...
Hijjah

Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Msimamo wa Uislamu juu ya Utumwa

- Watumwa walikuwa wakikamatwa na kutezwa nguvu bila kujali utu na ubinaadamu wao.

Soma Zaidi...
Jinsi ya kusherehekea siku ya idi katika uislamu

Uislamu umeweka taratibu maalumu za kuzifata katika kusherehekea siku ya idi.

Soma Zaidi...
Saumu (funga)

Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...