sunnah za swala

Sunnah za SwalaSunnah za Swala Vipengele vya sunnah katika swala ni vile ambavyo mwenye kuswali akivitenda husaidia sana kukuza daraja ya swala yake na kuipa nguvu na msukumo mkubwa wa kuiwezesha kufikia lengo lililokusudiwa kwa urahisi zaidi.

sunnah za swala

Sunnah za Swala
Sunnah za Swala Vipengele vya sunnah katika swala ni vile ambavyo mwenye kuswali akivitenda husaidia sana kukuza daraja ya swala yake na kuipa nguvu na msukumo mkubwa wa kuiwezesha kufikia lengo lililokusudiwa kwa urahisi zaidi.

Ama mwenye kuswali akiacha kipengele chochote katika vipengele vya sunnah, swala yake itakamilika iwapo atatekeleza vipengele vyote vya nguzo. Katika Hadith tumeona kuwa Mtume (s.a.w) katika swala yake pana vipengele vya ziada ya nguzo kama ifuatavyo:

1. Kuinua viganja vya mikono mkabala na mabega, usawa wa vigingi vya masikio wakati wa kuhirimia swala, kwenda kwenye rukuu, baada ya rukuu na baada ya kutoka kwenye Tahiyyatu ya kwanza.
2. Kusoma dua baada ya takbira ya kuhirimia.
3. Kuanza na afudhubillaah (kumlaani Shetani) kabla ya kuanza kusoma suratul-Fatiha.
4. Kuitikia Aaminhbaada ya kumaliza Suratul Fatiha.
5. Kusoma aya za Qur-an baada ya Suratul-Fatiha katika rakaa mbili za mwanzo. 6. Kuleta Tasbih, Tahmid na dua katika rukuu, itidali na sijda.
7. Kutoa takbira katika kubadilisha kitendo kimoja kuendea kingine isipokuwa tu kutoka kwenye rukuu kwenda kwenye itidali ndipo tunaposema: SamifAllahu liman hamidah - Rabbanaa lakal-hamdu.
8. Kukaa na kusoma Tahiyyatu kila baada ya rakaa mbili, kwa swala zenye rakaa zaidi ya mbili.
9. Kusoma dua baada ya kumswalia Mtume na kabla ya kutoa Salaam.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Jiunge nasi WhatsApp
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 2581

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉3 Dua za Mitume na Manabii    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Msimamo wa uislamu juu ya utumwa

Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Nguzo za udhu ni sita

Post hii itakufundisha kuhusu nguzo kuu sita za udhu.

Soma Zaidi...
Je manii ni twahara au najisi?

Post hii itakwenda kukufundisha hukumu ya manii kuwa ni twahara ama ni najis

Soma Zaidi...
Namna ya kuswali hatuwa kwa hatuwq

Post hii itakufundisha jinsi ya kuswali hatuwa kwa hatuwa.

Soma Zaidi...
Fadhila za usiku waalylat al qadir

Zijuwe fadhila za usiku wenye cheo kuliko nyusiku ya miezi 1000.

Soma Zaidi...
Kutoa zakat

Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...