2.
2. Kusoma Dua ya Kufungulia Swala
Kusoma dua ya kufungulia swala ni sunnah. Katika Hadithi ya Bukhari na Muslim iliyosimuliwa na Abu Hurairah (r.a), baada ya kuhirimia swala Mtume (s.a.w) alikuwa akileta dua ifuatayo: “wajahtu wajhi lilladhi fatwaras-samaawat wal-ardha hanifam-muslima wamaa ana minal-mushrikina. Inna swalatiy wanusukii, wamah-haya, wamaamatiy, lillahi rabil-alamiina laa sharikalahu wabidhalika umirtu wa-ana minal-muslimina.”“Nimeuelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi. Nimeacha dini za upotovu. Mimi si miongoni mwa washirikina. Hakika swala yangu (na ibada zangu zote) na uzima wangu na kufa kwangu (yote) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, bwana (Rabbi) wa walimwengu wote. Hana mshirika wake. Na haya ndio niliyoamrishwa na mimi ni wa kwanza walio jisalimisha kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu. (6:79, 162-163)
3. Kupiga Audhu Billah Kabla ya kuanza kusoma Qur-an ni amri ya Allah (s.w) kujikinga na sheitwani kama inavyodhihirika katika aya ifuatayo: 109 “Na ukitaka kusoma Qur-an piga Audhu billah (jikinge) kwa Allah (akulinde) na Sheitwani aliyefukuzwa (kwenye Rehema). (16:98) Hivyo tuanze kusoma Qur-an kwa kusema “A’udhu-billahi minash-shaytwanir- Rajiim” Najikinga kwa Allah na sheitwan aliyefukuzwa-kwenye Rehma yako
4. Kusoma Suratul-Fatiha Kusoma Suratul-Fatihah ni nguzo ya tatu ya swala na ndio nguzo kubwa ya swala. Tunasoma suratul-Fatiha kama ifuatavyo:- Bismillahir Rahmaanir Rahiim (1) Alhamdu liLLahi rabbil-’Aalamiin (2). Rrahmaanir Rahiim (3) Maaliki yaumiddiin (4) Iyyaakana ‘abudu waiyyaaka nasta‘iin (5) Ih dinasw-swiraatwal mustaqiim (6) Swiraatwa lladhiina an ‘amta ‘alaihim; ghairil maghdhuubi ‘alaihim wala dhw-dhwaaliin (7)
Tafsri:
(1) Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na mwenye kurehemu: (2) Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu, Mola wa Walimwengu wote: (3) Mwingi wa Rehema mwenye kurehemu (4) Mwenye kumiliki siku ya malipo: (5) Wewe tu ndiye tunayekuabudu, na wewe tu ndiye tunaye kuomba msaada: (6) Tuongoze njia iliyonyooka: (7) Njia ya wale uliowaneemesha; siyo (ya wale ) waliokasirikiwa, wala ya wale waliopotea
5. Kusoma Qur-an baada ya Suratul-Fatiha Katika rakaa ya kwanza na ya pili ni Sunnah baada ya kusoma Suratul-Fatiha kuleta Surah au aya nyingine za Qur-an:
Umeionaje Makala hii.. ?
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Lengo la funga ni kuwa mchamungu sasa ni kwa nini wafungaji hawalifikii lengo hili na kuwa wachamungu.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza jinsi ya kuozesha hatuwa kwa hatuwa. Pia utajifunza masharti ya kuoa na masharti ya kuolewa.
Soma Zaidi...Kuchukuwavudhu ni ibada, lakini pia ni matendo ya kuufanya mwilivuwe safi. Katika post nitakwenda kukifundisha namna ya kutia udhu katika uislamu.
Soma Zaidi...Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3:Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu mambo ambauo ni haramu kwa mtu asiye na udhu.
Soma Zaidi...