picha

DARSA ZA TAWHID

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

DARSA ZA TAWHID

 Tawhiid.
oKimaana: Ni Umoja au Upweke wa Mwenyezi Mungu (s.w).
oKimatumizi: Ni fikra, mtazamo wa kimapinduzi katika kumkomboa mwanaadamu na aina zote za utumwa wa kibinaadamu na kuwa mtumishi huru wa Muumba wake.

Aina za Tawhiid.
Kuna aina kuu tatu za Tawhiid kama zilivyoainishwa katika aya za Qur’an.
(i) Tawhid Al-Uluuhiyyah – Upweke wa Allah (s.w) katika Uungu wake. Nayo ni Kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) katika Uungu wake kwa kutokuwa na mungu mwingine yeyote wa kumuelekea kwa ibada au maombi isipokuwa yeye peke yake. Rejea Qur’an (2:163), (3:62) na (112:1-4).

(ii) Tawhiid Al-Asmaa Wassifaat – Upweke wa Mwenyezi Mungu (s.w) katika Majina na Sifa. Nayo ni kutomsifu Mwenyezi Mungu (s.w) kwa sifa za viumbe au majina ya viumbe na pia kutomsifu kiumbe yeyote kwa sifa za Mwenyezi Mungu (s.w). Rejea Qur’an (57:1-6) na (59:22-24).

(iii) Tawhiid Rabbuubiyya – Upweke wa Mwenyezi Mungu (s.w) katika Ubwana,Utawala na Mamlaka Yake. Kumpwekesha Allah (s.w) katika Ubwana na Utawala wake ni kutofuata na sheria na taratibu za maisha kinyume na zile alizoziweka yeye kwa kumfanya ndiye Mlezi, Mlinzi, Mwendeshaji wa kila kitu. Rejea Qur’an (4:59), (31:14-15), (25:52), (3:149), (3:100) na (5:57). bofya hapa


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: General Main: Post File: Download PDF Views 5307

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Dua za Mitume na Manabii     👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zinazofanana:

KUAMINI MALAIKA

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

Soma Zaidi...
HISTORIA YA UANDISHI WA HADITHI

Historia fupi ya uandishi wa Hadith za Mtume (s.

Soma Zaidi...
Je mahari inashusha hadhi ya mwanamke?

Je, Mahari inashusha hadhi ya mwanamke?

Soma Zaidi...