FAIDA ZA KITUNGUU THAUMU

Kitunguu thaumu ni katika viungo vya mboga na chakula. Karibia maeneo yote duniani wanatumia kitungiuu thaumu. Kitunguu thaumu huweza kutumika kikiwa kibichi. Wataalamu wa afya wanaeleza faida nyingi za kiafya. Wataalmu wa afya wametengeneza kidonge kwa kutumia vitunguu thaumu ili kuwezesha upatikanaji wa virutubisho vya mmea huu.

 

Kitunguu thaumu kina chembechembe nyingi ambazo ndizo husaidia katika tiba. Miongoni mwa chembechembe hizo ni chembechembe za salfa ziitwazo allicin. Allicin hupatikana kwenye kitunguu kibichi pindi kinapopondwa ama kutafunwa. Chembechembe nyingine ni kama  diallyl disalfide na s-allyl cysteine.

 

Zifuatazo ni faida za kiafya za kitunguu thaumu

  1. Kunapatikana virutubisho vingi ndani ya kitunguu thaumu kama vitamini B6, B1 na vitamini C.  madini ya calcium, copper, phosphoros, potassiumna selium.
  2. Hushusha presha ya damu (hypertsnsion). kitunguu thaumu sio kizuri kwa wenye presha ya kushuka, kwani itashuka sana.
  3. Hudhibiti cholesterol (kolesto) hivyo husaidia katika kuzuia hatari ya kupata maradhi ya moyo.
  4. Kitunguu thaumu kina antioxidant ambazo husaidia kupunguza hatari ya kupata maradhi ya kusahausahau
  5. Huimarisha mfumo wa kinga mwilini.
  6. Huondoa sumu za vyakula mwilini.
  7. Huimarisha afya ya mifupa.