JITIBU KWA TANGAIZI: faida za kiafya za tangaizi

Tangaizi ni katika mimea yenye asili na bara la asia hususan nchi ya China.

JITIBU KWA TANGAIZI: faida za kiafya za tangaizi

FAIDA ZA TANGAIZI

Tangaizi ni katika mimea yenye asili na bara la asia hususan nchi ya China. Mmea huu hutambulika kwa faida zake za kitiba toka zamani sana. Na karibia dunia nzima hutumia tangaizi kama tiba na kama kinywaji. Ndani ya tangaizi kuna chembechembe ziitwazo gingerol, hizi ndizo huipa tangaizi uwezo wake wa kitiba.

 

Unaweza kutumia tangaizi kwa kutafuna vipande vidogovidogo au kwa kutia kwenye  mboga. Pia unaweza kuweka kwenye chai ikiwa vipande vidogo au ikiwa imekauchwa na kusagwa kama ungaunga. Zipo njia nyingi za kutumia tangaizi. Zifuatazo ni katika baadhi ya faida za tangaizi iafya:-

 

  1. Tangaizi ni mujarabu sana katika kutibu kichefuchefu. Hususani kichefuchefu cha mimba. Kwa ujumla kichefuchefu huwapata sana wajawazito, na watu walofanyiwa upasuaji wa ndani. Lakini kinaweza kumpata mtu yeyote. Unaweza kutumia tangaizi kwenye chai, ama kutafuna vipande vidogo. Hakikisha unakula japo gram moja.
  2. Hupunguza maumivu ya misuli
  3. Hupunguza maumivu ya viungo
  4. Husaidia katika kushusha kiwango cha sukari. Hususan kwa wenye kisukari type 2. kwa kufanya hivi pia hupunguza athari ya kupata maradhi ya moyo
  5. Husaidia kwa wenye tatizo la kutokupata choo na kukosa hamu ya kula.
  6. Hupunguza maumivu ya tumbo la chango kwa wanawake.
  7. Hupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa saratani (cancer)
  8. Huimarisha afya ya ubongo
  9. Husaidia katika kuimarisha mfumo wa kinga za mwili.


                   



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 178


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-