FIQH 1.
FIQH
1.TWAHARA
Twahara ni neno la kiarabu lenye maana ya usafi au unadhifu. Na neno hili kisheria ni kuondoa yale yanayomzuilia mtu kuswali ambayo ni katika hdathi na najisi, kwa kutumia maji au vinavyosimama badala ya kukosekana kwa maji kama udongo.
Kuondoa najisi ni jambo la wajibu pindi mtu anapokumbuka na akiwa na uwezo wa kufanya hivyo. Kama aliposema Allah kumwambia Mtume (s.a.s): “na nguozako uzitwaharishe” (surat muzammil: 4). Na Mtume صليالله عليه وسلم amesema “haikubaliwi swala (iliyoswaliwa ) bila ya udhu”.
Kuwa twahara tofauti na kuwa ni jambo lililohimizwa sana kwenye uislamu hata Mtume صليالله عليه وسلم akasema: “uislamu ni usafi” ila pia kuna faida nyingi sana tunazipata kwa kutekeleza jambo hili:
1.Twahara ni sharti katika kuswihi kwa sala. Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Mtume صليالله عليه وسلم amesema:”haikubaliwi swala ya mtu aliyehuduthi (aliyejamba) mpaka atawadhe” (Bukhari na Muslim)
2.Allah amewasifia sana watu ambao wanakuwa twahara. Amesema Allah “hakika Allah anawapenda wenye kutubia na anawapenda wenye kuwa twahara” (Surat baqara aya 222).
3.Kuwa twahara ni sababu ya kutokuadhibiwa kaburini. Ni kuwa watu ambao hawajikingi na najisi kama mkojo na hawajitwaharishi wataadhibiwa makaburini. Imesimuliwa hadithi na Ibn Abas kuwa Mtume صليالله عليه وسلم alipita kwenye makaburi mawili kisha akasema : “hakika watu hawa (waliozikwa hapa ) wanadhibiwa, na si kwa makosa makubwa bali kwa hakika huyu mmoja alikuwa hajisafishi anapokojoa.….” (Ibn Majah N Abu daud na isnad ya hadithi ni sahihi)
Aina za twahara.
Basi tambua kuwa twahara ip katika makundi makuu mawili ambayo ni:
1.twahara haqiqiya: nayo ni ni kujitwaharisha na khabathi yaani najisi na inaweza kuwa kwenye mavazi au mwili.
2.Twahara hukmiyah: nayo ni kujitwaharisha na hadathi na hii inahusiana na mwili tu na aina hii imegawanyika katika makundi matatu ambayo ni:-
A)Twahara kubwa; ambayo ni kuonga (josho la kisheria)
B)Twahara ndogo; nayo ni kutawadha yaani udhu
C)Twahara iliyo badala ya aina mbili zilizotangulia nayo ni kutayamam, yaani kujitwaharisha kwa kutumia udongo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Hapa tunakwenda kuona jinsi ya kuzitathmini swala zetu.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza jinsi ya kuozesha hatuwa kwa hatuwa. Pia utajifunza masharti ya kuoa na masharti ya kuolewa.
Soma Zaidi...Katika post hii utajifunza maana ya twahara kiligha na kishria. Pia utajifunza umuhimu wake
Soma Zaidi...Hapa utajifunza sera za kiuchumi katika uchumi wa kiislamu. Hapa utajifunza sera kuu tatu za uchumi wa kiislamu.
Soma Zaidi...Kwa nini Lengo la Zakat na Sadaqat Halijafikiwa katika Jamii yetu?
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukugundisha kuhusu swala ya ijumaa taratibu zake na jinsi ya kuiiswali.
Soma Zaidi...