image

Uyoga (mushrooms)

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula uyoga

Uyoga (mushroom)

Uyoga pia ni katika vyakula vya asili, ijapokuwa upatikanaji wake umekuwa mchache siku hizi. Shukrani ziwaendee wataalamu wa kilimo, kwa sasa tunaweza kuzipata mbegu za uyoga kutoka maabara na kulima uyoga popote pale. Wataalamu wa mimea wanaamini kuwa uyoga si katika mimiea kwani uyoga upo katika kundi la viumbe liitwalo fungi (kingdom fungi). ila tunapozungumzia vyakula uyoga tunauweka kwenye kundi la mbogamboga. Uyoga una virutubisho vingi na vizuri kwa afya.

 

Kulinda mwili zidi ya cancer, Kama ilivyokuwa kwenye matunda na mboga zingine kuwa kuna antioxidant ambayo hii ni chembechembe inayopambana na sumu na kemikali ambazo zinaweza kuathiri seli za mwili wako. Basi kwenye uyoga pia kuna antioxidant kama iliyo karoti na matunda mengine tuloona hapo juu. Hii husaidia kwa kiwango kikubwa kupambana na kuuwa seli za kansa au saratani ambazo zinatengenezwa mwilini.

 

Mna kwenye uyoga madini yanayoitwa selenium, madini haya huwezi kuyapata kwenye matunda mngi sana na mbogamboga nyingi lakini haya utayapata kwa urahisi kwenye uyoga. Madini haya husaidia katika kuuwa seli sa saratani, pia kuzuia kuota kwa uvimbe unaosababishwa na saratani na aina zingine za vimbe.

 

Uyoga una vitamin D, ambavyo hivi pia husaidia katika kupambana na kuthibiti kukuwa kwa seli za saratani mwilini. Vitamin D husaidia katika utendaji mwema wa kazi za DNA. Itambulike kuwa saratani huanza kuathiri DNA ndio baadae huendelea kukuwa ndani ya mwili na baadae kuathiri sehemu za mwili. Hivyo uyoga una chembechembe hizi ambazo husaidia katika kupamba na nsa saratani.

 

Uyoga husaidia katika kuthibiti na kupamabana na kisukari hususan type 2 diabetes. Wataalamu wa afya wanatueleza kuwa ulaji wa vyakula vyenye kambakamba (fiber) husaidia katika kushusha kiwango cha sukari kwenye damu. Hivyo husaidia katika kuimarisha afya ya itengenezwaji wa insulin.

 

Husaidia katika kuimarisha afya ya moyo, uwepo wa lkambakamba, madini ya potassium pamoja na vitamin C husaidia kwa kiwango kikubwa katika kuimarisha afya ya moyo (cardiovascular health). ulaji wa vyakula vyenye madini ya potassium kwa wingi pamoja na sodium kwa kiwango kidogo husaidia katika kupunguza shinikizo la damu hivyo husaidia kwa wale wenye presha ya kupanda ya damu.

 

Husaidia katika kuimarisha mfumo wa kinga mwilini (immune system). madini ya selenium yaliyomo kwenye uyoga kusaidia katika kushawishi na kustimulate mfumo wa afya mwilini katika kupambana na wadudu wavamizi. Madini haya husaidia katika kusahwishi T-cell au CD4 katika kupambana na wadudu wavamizi kama bakteria, virus na fangas. Beta-glucan inayopatikana kwenye ukuta wa seli za uyoga husaidia katika kuufanya mwili upambane vyema na wavamisi na kupamba nna na vijidudu vya maradhi.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1669


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

Faida za kiafya za kula Tango
Soma Zaidi...

JITIBU KWA TANGAIZI: faida za kiafya za tangaizi
Tangaizi ni katika mimea yenye asili na bara la asia hususan nchi ya China. Soma Zaidi...

Vyakula vya vitamini C na faida zake
Soma Zaidi...

Faida za kula tikiti
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula tikiti Soma Zaidi...

Vyakula kwa wagonjwa wa sukari na utaratibu wao wa lishe
Post hii inakwenda kukufundisha utaratibu wa lishe kwa wagonjwa wenye kisukari pamoja na vyakula salamakwao. Soma Zaidi...

Faida za kula apple (tufaha)
Posti hii itakwende kukueleza kuhusu faida za kula apple na umuhimu wake kiafya Soma Zaidi...

Fahamu tiba ya lishe ya ugonjwa wa kisukari
Post hii inahusu zaidi tiba ya lishe ya ugonjwa wa kisukari ni tiba ambayo utumiwa sana na wagonjwa wa kisukari na walio wengi na wamefanikiwa kupona Soma Zaidi...

FAIDA ZA KULA ZABIBU
Somo hili litakwenda kukueleza kuhusu faida za kula zabibu na umuhimu wake kiafya Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Fyulisi
Soma Zaidi...

Vijuwe virutubisho vilivyomo kwenye parachichi.
Posti hii inahusu zaidi virutubisho vilivyomo kwenye parachichi, tunajua sana kuwa parachichi ina virutubisho vingi ambavyo vinaweza kuleta faida nyingi kwenye mwili kama yalivyo matunda na vyakula vingine. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Zaituni
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kunywa maziwa
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kunywa maziwa Soma Zaidi...