vyakula vya kuongeza damu, dalili zake na sababu za upungufu wa damu

vyakula vya kuongeza damu, dalili zake na sababu za upungufu wa damu

Zijuwe sababu za upungufu wa damu, dalili za upungufu wa damu na kazi za damu mwilini,n avyakula vya kuongeza damu

vyakula vya kuongeza damu, dalili zake na sababu za upungufu wa damu

Upungufu wa damu, dalili zake na vyakula vya kuongeza damu


VYAKULA VYA KUONGEZA DAMU



Damu ni tishu iliyo katika kimiminika. Katika miili yetu damu ina kazi ya kusafirisha viinilishe na hewa ya oksijeni na kuondoa hewa chafu ya kabonidaiyoksaidi mwilini. Pia urekebishwaji wa joto na usafirishwaji wa homoni ndani ya mwili hutegemea damu. Kwa ufupi damu in akazi nyingi. Upungufu wowote wa damu mwilini unaweza kuleta athari nyingi mbaya za kiafya mwilini. Makala hii inakwenda kukueleza njia ya kuongeza damu kwa haraka.


Kazi za damu mwilini
1.Kusafirisha viinilishe kutoka katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwenda maeneo mbalimbali ya mwili.
2.Kusafirisha hewa ya oksijeni kutokakwenye mapafu kwenda maeneo mengine ya mwli.
3.Kusafirisha hewa ya kabonikaiyoksaidi kutoka kwenye seli na kpeleka kwenye mapafu kwa ajili ya kutolewa nje
4.Kudhibiti joto la mwili kwa kulipooza inapohitajika na kuliongeza inapohitajika
5.Kusafirisha homoni kwenda maeneo mbalimbali ya mwili.


Vyakula vya kuongeza damu mwilini
1.Nyama nyekundu kama nyama ya ng’ombe, mbuzi. Kondoo
2.Maini
3.Nyama ya figo
4.Mboga za rangi ya kijani kama mchicha na apinachi
5.Maharagwe
6.Kunde
7.Mayai
8.Nafaka nyinginezo
9.Njegere
10.Koeosho na karanga
11.Samaki
12.Nyama ya ndege
13.Karoti
14.Matikiti
15.Zabibu
16.Viazi vitamu
17.Matunda yenye uchachu kama machungwa, ndimu na limao.
18.Polipili nyekundu


Dalili za kupungua kwa damu mwilini
1.Uchovu wa hali ya juu
2.Udhaifu wa mwili
3.Ngozi kuwa na rangi ya njano au mauko
4.Kupumua kwa shida
5.Mapigo ya moyo kutokuwa ya kawaida
6.Kizunguzungu na kichwa kuhisi chepesi
7.Maumivu ya kifua
8.Miguu na mikono kuwa ya ubaridi
9.Maumivu ya kichwa



Sababu za upungufu wa damu mwilini
1.Upungufu wa madini ya chuma mwilini
2.Upungufu wa vitamini A na B-12 mwilini
3.Maradhi kama HIV, UKIMWI, saratani, mardhi ya figo haya huweza kuleta upungufu wa damu
4.Mfumo wa kinga mwilini kuuwa na kuharibu seli hai nyekundu (autoimmune)
5.Uharibifu wa seli hai nyekundu kufanyika kwa haraka kuliko utengenezwaji.
6.Kuwa na maradhi ya sickle cell




                   


Bongoclass
Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya hapa chini kuipakua sasa!

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Vyakula Main: Afya File: Download PDF Views 3048

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰2 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰3 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰4 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Kazi kuu tatu za Vitamini C mwilini
Kazi kuu tatu za Vitamini C mwilini

Vitamini C tunaweza kuvipata kwenye matuinda kama machunwa vina kazi kuu tatu ambazo ni hizi hapa

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za topetope (accustard apple/sweetsop)
Faida za kiafya za topetope (accustard apple/sweetsop)

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula topetope

Soma Zaidi...
Nini maana ya protini
Nini maana ya protini

Unaijuwa maana ya virutubisho vya protini, na kazi zake mwilini. Soma zaidi hapa

Soma Zaidi...
FAIDA ZA MATUNDA
FAIDA ZA MATUNDA

Somo hili linakwenda kukuletea faida za MATUNDA mbalimbali na mboga, upatikanaji wake na faida zake kiafya. Pia utakwenda kuona MATUNDA na mboga ambayo Ni kinga dhidi ya maradhi hatari Kama kisukari, saratani, maradhi ya moyo na mfumo wa fahamu pamoja na

Soma Zaidi...
Mafidodo (mafindofindo)  au tonsils kweye koo je inaweza ikawa Ni moja kati ya dalil za ukimwi
Mafidodo (mafindofindo) au tonsils kweye koo je inaweza ikawa Ni moja kati ya dalil za ukimwi

Tezi za lymph huanza kuonyesha dalili za kuwa mwili upo katika mapambano dhidi ya vijidudu vya maradhi. Ishara ni pale utakapoona tezi za lymph zina maumivu. Tezi hizi hupatikana kwenye mapaja, kwapa nashingo.

Soma Zaidi...
Sababu za maumivu ya tumbo baada ya kula
Sababu za maumivu ya tumbo baada ya kula

Zijuwe sababu kuu za kuwepo kwa maumivu ya tumbo baada ya kula chakula

Soma Zaidi...
Ndizi (banana)
Ndizi (banana)

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula ndizi

Soma Zaidi...
Faida za kula kunde, maharage, njegere, mbaazi na njugu mawe
Faida za kula kunde, maharage, njegere, mbaazi na njugu mawe

Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula kunde, maharage, njegere, mbaazi na njugu mawe

Soma Zaidi...