TATIZO LA KUVIMBA KWA USO NA MIGUU KWA WAJAWAZITO

KUVIMBA VYA MIGUU KWA WAJAWAZITO Kuvimba kwa miguu ni hali inayowapara wengi katika wajawazito.

TATIZO LA KUVIMBA KWA USO NA MIGUU KWA WAJAWAZITO

KUVIMBA VYA MIGUU KWA WAJAWAZITO
Kuvimba kwa miguu ni hali inayowapara wengi katika wajawazito. Kitaalamu hali hii hutambulika kama odema. Wakati mwingine si miguu tu ndio huvimba bali mikono, nyayo na uso huweza kuvimba. Ijapouwa huku kukuvimba kwa ghafla kwa uso na mikono ni dalili ya maradhi mengine kama preeclampsia.

Hali hii ya kuvimba kwa miguu huweza kuwapata wanawake katika kipindi chote cha ujauzito, iwe wajauzito ulio mchanga, ama kipindi cha katikati cha ujauzito ama kipindi cha mwisho cha ujauzito. Katika hali ya kawaida kuvimba kwa miguu kwa wajawazito sio jambo la kusumbua kiafya yaani kusema kuwa ni tatizo kubwa. Hapana hii ni kawaida kwa wajawazito.

Kuvimba huku kunaweza kuwa ni tatiko kama kutaweza kuambatana na baadhi ya matatizo mengine ya kiafya kama maumivu makali ya kicha, kizunguzungu, kutokwa na damu, kushinwa kuona kwa usahihi ama kushinwa kupumua ama kupumua kwa taabu, hali hizi kuweza kuashiria hatari. Ni vyema mjamzito awahi kituo cha afya kama ana hali hizi.

Sababu za kutokea kwa vimbe hizi ni mabadiliko ya mwilini yanayopatikana wakati wa ujauzito. Kuongezeka kwa damu mwilini na kuongezeka kwa mapigo ya moyo huweza kuchangia zaidi hali hii. Halikadhalika ongezeko la homoni maalumu zinazotolewa wakati wa ujauzito. Haya yote kwa pamoja huchangia kutokea hali hizi za kuvimba.

Tofauti na sababu hizi pia zipo nyingine kama mabadiliko ya hali ya hewa. Hapa tunazungumzia joto, ambalo pia ni sababu ya kuvimba. Sababu nyingine ni kutokunywa maji ya kutosha, matatizo ya homoni yaani homone imbalance. Kukaachini kwa muda mrefu ukaaji wa kukalia miguu. Ama kusimama kwa muda mefu.

Kupunguza ama kuepuka hali hii ni vyema kufanya mazoezi ya mara kwa mara, kukaa kivulini, kulalia upande kwa kushoto unapolala. Hakikisha unakula mlo kamili, hakikisha kuwa unakunywa maji ya kutoka kwa siku. Na hata ukizidisha ni faida kwako. Epuka kusimama kwa muda mrefu ama kukaa kwa kukalia mguu. Epuka kukaa kwa muda mrefu kwa staili moja. Kuna matatizo mengu ya kiafya yanayoambatana na ujauzito, ni vyema mjamzito akiwa makini.





                   



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 796


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-