image

Dua Sehemu ya 02

Zijuwe nyakati ambazo dua inakubaliwa kwa haraka zaidi. Zijuwe nyakati ambazo ukiomba dua hitakubaliwa.

Dua Sehemu ya 02

NYAKATI AMBAZO DUA HUJUBIWA.
1.Theluthi ya mwisho ya usiku. Huu ni usiku wa manane usiku mkubwa. Muda huu mweye kuomba dua katu haiwezi kurudi kama anavyosimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema "‏ يَنْزِلُ رَبُّنَا كُلَّ لَيْلَةٍ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا حِينَ يَبْقَى ثُلُثُ اللَّيْلِ الآخِرُ فَيَقُولُ مَنْ يَدْعُونِي فَأَسْتَجِيبَ لَهُ وَمَنْ يَسْأَلُنِي فَأُعْطِيَهُ وَمَنْ يَسْتَغْفِرُنِي فَأَغْفِرَ لَهُ ‏" “anashuka Mola wetu aliye tukuka kuja mbingu ya dunia kila usiku pindi inapobaki theluthi ya usiku ya mwisho kisha husema ‘nani ataniomba nimjibu maombi yake, nani antaniomba nimpe na nani ataniomba msamaha nimsamehe”. (amepokea Bukahari, muslim na wengine).

2.Baada ya swala za faradhi. Anayetaka kuomba dua basi aombe baada ya kuswali swala ya faradhi, dua yake itajibiwa. عَنْ أَبِي أُمَامَةَ، قَالَ قِيلَ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَىُّ الدُّعَاءِ أَسْمَعُ قَالَ ‏"‏ جَوْفُ اللَّيْلِ الآخِرُ وَدُبُرَ الصَّلَوَاتِ الْمَكْتُوبَاتِ ‏"‏ Amesimulia Abuu Umama رضىالله عنه kuwa aliulizwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم ‘dua gani husikulizwa (zaidi na Allah? Akasema:) usiku mkubwa (theluthi ya mwisho ya usiku) na baada ya swala za faradhi’”. (amepokea tirmith kwa isnad sahihi).

3.Kati ya adhana na iqama. Huu ni muda unaopatikana baada ya kuadhiniwa na mpaka kukimiwa kwa swala. Hapa mwenye kuomba dua itakuwa ni yenye kujibiwa. Amesimulia Anas رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “hairudishi (haiachi kujibiwa dua) kati ya adhana na iqama”. (amepokea Abuu Daud, Nisai na tirmith kwa isnad sahihi).

4.Wakati wa kusujudi. Hii ni dua inayoomwa wakati mtu akiwa amesujudi, dua hii pia ni yenye kujibiwa. Amesimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “muda ambao mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake ni pale akiwa amesujudi. Basi zidisheni dua (muda huu) na uweni na uhakika kuwa mtajibiwa. (amepokea Muslim na Daud).

5.Muda wa kukutana majeshi kwenye jihad, muda wa kunyesha kwa mvua, muda wa kukimiwa kwa swala na na muda wa kuiona alkaba. Amepokea Abuu Umamah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema: “hufunguliwa milango ya mbinguni na hujibiwa dua katika maeneo manne (nyakati): muda wa kukutana safu katika jihadi, muda wa kunyesha kwa mvua, muda wa kukimiwa kwa swala na muda wa kuiona alkaba”. (amepokea Tabrany).

6.Siku ya ijumaa. Siku ya ijumaa kuna muda ambao dua hujibiwa bila ya tatizo. Muda huu ni mchache sana na hakuna anaoujua. Zipo riwaya nyingi sana zinataja muda huu. Ila kuna riwaya zinaonesha muda huu ni baada ya swala ya al-’asr mpaka magharib. Ila ukweli ni kuwa muda huu ni mchache sana na haujulikani, jambo la msingi ni kujitahidi kumuomba Allah siku ya ijumaa yote huenda muda huo ungeupata.

HALI AMBAZO MTU AKIOMBA DUA ITAJIBIWA.
1.Dua ya kumuombea aliye mbali. Chukulia mfano una ndugu yako yupo nchi nyingine ama mji mwingine kisha ukamkumbuka na ukataka kumuombea dua, basi dua hii itajibiwa tu. Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “hakika dua iliyo nyepesi (na haraka ) kujibiwa ni dua ya mtu kumuombea aliye mbali” (amepokea Abuu Daud na Tirmidh kwa isnad sahihi). Pia amesimulia Abuu Dardaa رضىالله عنه kuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “dua ya mtu muislamu ni yenye kujibiwa anapomuombea ndugu yake aliye mbali. Juu ya kichwa chake kuna Malaika anaitikia ‘aamiin’ na wewe upate mfano wa wake”. (amepokea Ahmd na Muslim).

2.Dua ya mzazi, msafiri na mwenye kudhulumiwa. Hali za watu watatu hawa wakiomba dua Allah atajibu dua zao bila ya shaka. Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema ‏ "‏ ثَلاَثُ دَعَوَاتٍ يُسْتَجَابُ لَهُنَّ لاَ شَكَّ فِيهِنَّ دَعْوَةُ الْمَظْلُومِ وَدَعْوَةُ الْمُسَافِرِ وَدَعْوَةُ الْوَالِدِ لِوَلَدِهِ

3.“dua za watu watatu (hawa) ni zenye kujibiwa na hakuna shaka juu ya hili: dua ya mzazi, msafiri na mwenye kudhulumiwa”. (amepokea Abuu Daud, Ahmad na Tirmidh kwa sanad sahihi).

4.Dua ya mwenye swaum (funga), imamu muadilifu, na mwenye kudhulumiwa. Watu hawa dua zao zitajibiwa tu, kingozi muadilifu, mtu aliyekuwa kwenye funga na kabla hajafuturu na mtu aliyedhulumiwa. Amesema Mtume صلّي الله عليه وسلّم watu watatu dua zao hazirudi: mwenye funga mpaka afutauru, imamu muadilifu (kiongozi muadilifu), na mwenye kudhulumiwa.…….” (amepokea tirmidh kwa isnad sahihi).

SIFA ZA (MANENO NA MATAMSHI YA) DUA YENYE KUJIBIWA.
Hapa tutaona dua iliyo katika sura ambayo Allah ataijibu. Dua zenye kujibia wakati mwingine zina sura yake na sifa zake katika maneno na matamshi. Hebu tuone sifa hizo.

1.Dua ya nabii Yunusi. Mwenye kuomba dua na akatumia maneno aliyoyasema nabii Yunusi (amani ishuke juu yake) dua hii ni yenye kujibiwa. Amesema mtume صلّي الله عليه وسلّم “dua ya nabii Yunus pindi alipokuwa kwenye tumbo la samaki (aliseme) ‘LAA LILAAHA ILLAA ANTA, SUBHAANAKA INII KUNTU MINADHWALIMIINA’ hakika hataomba mtu muislamu dua kwa kutumia maneno haya kitu chochote isipokuwa atajibiwa na Allah”. (amepokea tirmidh).

2.Kuomba dua kwa kutumia jina la Allah lililo kubwa. Allah ana majina mengi na mazuri. Lakini katika majina hayo lipo ambalo ni kubwa na ukiomba dua kwalo lakina utajibiwa. Kwa ufupi ni kuwa jina hili limefichwa na hakina yeyote anayelijuwa. Ila mtume ametowa ishara ya kuonesha wapi linapatikana na maneno gani mtu atumie kulipata jina hilo. Amesema mtume صلّي الله عليه وسلّم “jina kubwa la Allah lipo kwenye aya sita za mwisho za surat hashri. (amepokea Dilamy kutoka kwa Ibn ‘Abas). Pia katika mapokezi mengine ya Tabrany kutoka kwa Ibn ‘Abas kuwa mtume amesema jina kubwa lipo kwenye aya ya 20 ya surat al-imran. Na pia zipo hadithi nyingi sana zinazoashiri wapi jina hilo lipo. Nitaleta chache tuu.

i) Aisha رضىالله عنها aliomba dua hii “ ALLAHUMMA INII AD’UKA LLAHA WA-AD’UKAR-RAHMANA, WA-AD’UKAL-BARRAR-RAHIIMA, WA-AD’UKA BIASMAAIKAL-HUSNAA KULLIHAA MAA ‘ALIMTU WAMAA LAM A’ALAM AN TAGHFIRA LII WATARHAMNII” Mtume akacheka kisha akasema “hakika jina kubwa lipo ndani ya dua hii. (amepokea Ibn Maajah kutoka kwa ‘Aisha) hadithi hii ni ndefu nimeikatisha na kuchukua hiyo dyua tu.

ii)hadithi ya Anasرضىالله عنهkuwa” عَنْ أَنَسٍ، قَالَ دَخَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم الْمَسْجِدَ وَرَجُلٌ قَدْ صَلَّى وَهُوَ يَدْعُو وَيَقُولُ فِي دُعَائِهِ اللَّهُمَّ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ الْمَنَّانُ بَدِيعُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ ذَا الْجَلاَلِ وَالإِكْرَامِ ‏.‏ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ تَدْرُونَ بِمَ دَعَا اللَّهَ دَعَا اللَّهَ بِاسْمِهِ الأَعْظَمِ الَّذِي إِذَا دُعِيَ بِهِ أَجَابَ وَإِذَا سُئِلَ بِهِ أَعْطَى ‏"amesimulia Anas رضىالله عنه kuwa alikuwa amekaa na mtume صلّي الله عليه وسلّم wamekaa msikitini na kulikuwa na mtu mmoja anaswali kisha akaomba dua kwa kusema “ ALLAHUMMA ANNII AS-ALUKA BIANNALAKAL-HAMDA, LAA ILAAHA ILLA ANTAL-MANNAANU BADI’US-SAMAAWATI WAL-ARDH YAA DHALJALALI WAL-IKRAM YAA HAYYU YAA QAYYUUM” akasema Mtume صلّي الله عليه وسلّم umemuomba Allah kwa jina lake kubwa ambalo anapoombwa kwalo atajibu”. (amepokea tirmidh kwa isnad gharib).

Iii)amesimulia Abdillah Ibn Buraydah رضىالله عنه kutoka kwa baba yake kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم alimsikia mtu mmoja akisema “ALLAHUMMA INNIASALUKA BIAN-ASHHADU ANNAKA ANTALLAHU LAA ILAAHA ILLA ANTA. AL-AHADUS-SWAMADUL-LADHII LAMYALID WALAM YUULAD, WALAM YAKUN LAHU KUFWAN AHAD” akasema Mtume صلّي الله عليه وسلّم hakika umemuomba Allah kwa jina lake kubwa ambalo akiombwa hutoa na akiombwa dua hujibu. (amesimulia Abuu Daud,tirmidh,Ibn Maajah na Ibn Hiban).

Iv). Mtume amesema اسْمُ اللَّهِ الأَعْظَمُ فِي هَاتَيْنِ الآيَتَيْنِ ‏{وَإِلَهُكُمْ إِلَهٌ وَاحِدٌ لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الرَّحْمَنُ الرَّحِيمُ}‏ وَفَاتِحَةِ سُورَةِ آلِ عِمْرَانَ ‏"‏Jina kubwa la Allah linapatikana kwenye aya hizi‘ waillahukum ilahu wahidu laa ilaaha illa huwar-rahmanir-rahiim’ na mwanzoni mwa surat al ‘Imran

3.dua ya Mtume صلّي الله عليه وسلّم ni yenye kujibiwa. "‏ لِكُلِّ نَبِيٍّ دَعْوَةٌ مُسْتَجَابَةٌ وَإِنِّي اخْتَبَأْتُ دَعْوَتِي شَفَاعَةً لأُمَّتِي وَهِيَ نَائِلَةٌ إِنْ شَاءَ اللَّهُ مَنْ مَاتَ مِنْهُمْ لاَ يُشْرِكُ بِاللَّهِ شَيْئًا ‏"‏ Katika hadithisahihi mtume amesema Nabii yeyote ameomba dua yake na akajibiwa. Na nikaifanya dua yangu mimi ni shifaa kwa umati wangu sikku ya qiama. (amepokea Bukhari, Muslim na tirmidh kutoka kwa Anas).

4.Dua wakati wa raha hujibiwa wakati wa shida. Hii ni sifa ya dua yenye kujibiwa mbayo watu wengi hatujui. Nikuwa pindi unapopata neema na raha hapo ndipo pa kumuomba Allah na Allah atakujibu wakati unapopata matatizo kwa kukufariji na kukuondlea matatizo. Amesimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema "‏ مَنْ سَرَّهُ أَنْ يَسْتَجِيبَ اللَّهُ لَهُ عِنْدَ الشَّدَائِدِ وَالْكُرَبِ فَلْيُكْثِرِ الدُّعَاءَ فِي الرَّخَاءِ ‏" ‏ “mwenye kutaka kujibiwa dua yake wakati akiwa na shida basi azidishe kumuomba Allah wakati wa raha”. (amepokea Tirmidh kwa isnad gharib). Na katika mapokezi mengine amesema Mtume صلّي الله عليه وسلّم "‏ مَنْ سَرَّهُ أَنْ يَسْتَجِيبَ اللَّهُ لَهُ عِنْدَ الشَّدَائِدِ وَالْكُرَبِ فَلْيُكْثِرِ الدُّعَاءَ فِي الرَّخَاءِ ‏" “Mwenye kupenda kujibiwa dua zake wakati wa shida na taabu basi na azidishe dua wakati wa raha” (amepokea tirmidh)



         › WhatsApp ‹ Whatsapp





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 703


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Kitabu cha Afya 02
Kama tulivyosema hapo juu kuwa afya ni kuwa mzima kimwili na kiakili. Soma Zaidi...

TAHADHARI KWENYE VYAKULA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Dhana ya uzazi wa mpango na historia yake duniani
Soma Zaidi...

darasa la lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...

dondoo 100 za Afya
Basi tambua haya;- 21. Soma Zaidi...

YANAYOATHIRI AFYA KATIKA MAZINGIRZ
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

magonjwa na lishe
3. Soma Zaidi...

AFYA YA UZAZI (UJAUZITO, KULEA WATOTO, AFYA YA MIMBA NA MTOTO, MAGONJWA YA KINAMAMA NA WANAUME)
Soma Zaidi...

MARADHI YASABABISHWAYO NA HALI ZA MAISHA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Kujiepusha na Vishawishi vya Zinaa
Kujiepusha na Vishawishi vya ZinaaKatika macho ya sheria kitendo cha zinaa kinahesabiwa pale wanapokutana kimwili mwanamume na mwanamke nje ya ndoa. Soma Zaidi...

UTAMBUE UGNJWA WA UTI DALILI ZAKE, CHANZO NA TAHADHARI DHIDI YAKE
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Fahamu mtindo mzuri wa maisha
Postei hizi inahusu zaidi mtindo mzuri wa maisha, yaani mtu ale ki vipi au afanyeni nini ili kuweza kuboresha afya yake. Soma Zaidi...